Fasili · 1/6
Lugha ya 'wachache' au ya 'kimaeneo' ni nini?
Neno "lugha ya wachache" linahusu aina mbili za hali za wazungumzaji:
- wazungumzaji wa lugha ambazo matumizi yake yanapungua na/au yanaelekea kutoweka. Idadi ya wazungumzaji inapungua, lugha hairithishwi au hairithishwi vya kutosha kwa vizazi vipya na kwa muda mrefu lugha yenyewe iko hatarini kutoweka.
Kiayalandi, ingawa ni lugha rasmi ya Jamhuri ya Ayalandi pamoja na Kiingereza, ni mfano wa hali hiyo ambapo idadi ya wazungumzaji wake imepungua kwa kutia wasiwasi.
- wazungumzaji wa lugha ambayo haijapewa haki yoyote, au haki za kutosha – kwa mfano kiwango cha chini cha hadhi rasmi ya pamoja – katika eneo ambako imezungumzwa kijadi. Lugha ya Kijerumani inayozungumzwa nchini Denmaki, huko Jutland Kusini, haitumiki katika nyanja za umma wala katika machapisho rasmi, na kuijua lugha hii si sharti la kupata nafasi katika utumishi wa umma.
Kwa mujibu wa ufafanuzi huu, hatutofautishi kati ya misemo 'lugha ya wachache' na 'lugha ya kimaeneo'.
Msemo 'lugha ya kimaeneo' mara nyingi hutumiwa kurejelea lugha zinazozungumzwa
katika dola zile ambazo, kwa sababu za kisiasa, hazitaki kutumia neno 'wachache'.
Kijerumani cha Alsace (Ufaransa) kinaitwa lugha ya 'kimaeneo' nchini Ufaransa wakati aina ya Kijerumani ya Jutland Kusini (Denmaki) inaitwa lugha ya 'wachache' nchini Denmaki.